Wednesday, September 21, 2011

WAKAZI JIJINI WATAKA SERIKALI ITIMIZE WAJIBU WAKE!

Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam, wameishauri serikali kutimiza wajibu wake ipasavyo kwa kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu matatizo mbalimbali yanayolikabili taifa ikiwemo suala zima la ufisadi.

Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema serikali haina budi kufanya maamuzi sahihi na yakudumu katika kushughulikia kero mbalimbali zinazojitokeza siku hadi siku kabla hazijaleta athari kubwa kwa taifa.

No comments:

Post a Comment