Friday, May 13, 2011

WAMILIKI WA NYUMBA ZILIZOBOMOLEWA NA MABOMU GONGOLAMBOTO WAOMBA UJENZI WA NYUMBA ZA FIDIA KINYELEZI UFUATE HAKI!

 Moja ya nyumba iliyobomolewa na milipuko ya mabomu hayo wakati wa maafa hayo yaliyotokea Gongolamboto
                             Mabaki ya bomu yaliyolipuka kutoka kambi ya jeshi Gongolamboto
Baadhi ya wakazi wa Gongolamboto wakiangalia moja ya nyumba iliyoharibiwa na milipuko ya mabomu.

Baadhi ya wamiliki ambao nyumba zao zilibomoka baada ya kulipukiwa na mabomu eneo la Gongolamboto wameiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha inasimamia ipasavyo zoezi la ujengaji nyumba za fidia ili kila muathirika apate haki yake kuendana na tathimini ilyofanywa.



Wakizungumza katika mahojiano maalum na kituo hiki, wamiliki hao wamesema kwa kuwabaadhi yao walikuwa na mali zingine kwenye nyumba zao kuna haja ya serikali kuliona hilo ili hatimaye wafidiwe ikiwemo kupewa viwanja vya barabarani.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam SAIDI MECKY SADICK amesema wakazi wa Gongolamboto ambao nyumba zao zilivunjwa kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya jeshi Gongolamboto watajengewa nyumba zao eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment