Friday, May 13, 2011

DK. ALI MOHAMED SHEIN ASEMA MAZINGIRA YA ZANZIBAR YANARUHUSU UWEKEZAJI!

                                                    DK. ALI MOHAMED SHEIN
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. ALI MOHAMED SHEIN amesema mazingira ya Tanzania visiwani yanaruhusu uwekezaji katika Sekta mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na Sekta ya Utalii.



Rais Shein aliyasema hayo wakati alipotembelewa na Balozi wa Urusi Nchini Tanzania BWANA ALEXANDR RANNIKH ikulu Mjini Zanzibar.


Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Mamlaka yake ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), imekuwa ikichukua juhudi za makusudi za kuhakikisha inatoa vipaumbele vyote kwa wawekezaji kutoka sehemu mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na kuondoa urasimu kwa wawekezaji.

Aidha, Dk. Shein alitoa pongezi kwa nchi ya Urusi kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa karibu kati yake na Zanzibar na kueleza kuwa Urusi ni miongoni mwa nchi tatu za mwanzo kufungua Ubalozi wake hapa Zanzibar mara tu baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964.


Nae Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Alexandr Rannikh alimueleza Dk. Shein azma ya nchi yake kuekeza hapa Zanzibar katika sekta mbali mbali za kiuchumi, utalii na biashara.

No comments:

Post a Comment