Monday, May 16, 2011

WAKAZI UBUNGO KISIWANI HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MILIPUKO!

Wakazi wa Ubungo Kisiwani, Kata ya Mabibo, Jijini Dar es salaam, wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kufuatia kituo cha kusukuma maji taka kutoka hostel za Mabibo kuelekea kwenye mabwawa ya kusafishia maji taka kutofanya kazi ipasavyo.



Afisa Afya Mkuu wa Wizara ya Afya, BARTHLOMAYO NGAEJE, amesema kufuatia kituo hicho kutopeleka maji sehemu husika hali hiyo inasababisha maji taka hayo kuelekea kwenye mto kilungule ambao hutumiwa na wakazi wa eneo hilo kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na umwagiliaji wa bustani za mbogamboga.


Kwa upande wake Afisa Afya mazingira, MARIAM MAHAMUDU, amewataka wananchi kuwa makini na bidhaa wanazotumia kutokana na baadhi ya bidhaa hizo kutoka katika mazingira ambayo si salama na yanahatarisha afya zao.

No comments:

Post a Comment