Monday, May 16, 2011

SHULE YA MSINGI VISEGESE KISARAWE YAOMBA MADARASA YAKARABATIWE!

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Visegese wilayani Kisarawe ameiomba serikali kuikarabati paa la shule hiyo lililoezuliwa na upepo na kusababisha madarasa mawili kuanguka hali inapelekea wanafunzi wa shule hiyo kusoma katika mazingira magumu.


Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo hiki, Mwalimu Mkuu huyo JOHN MICHAEL amesema kwa sasa wanalazimika kuwaweka wanafunzi zaidi ya 80 katika darasa moja kufuatia kuanguka kwa madarasa hayo.

No comments:

Post a Comment