Friday, May 13, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE ARUHUSU TATHIMINI YA RUSHWA NCHINI IWEKWE WAZI!

                                                     Waziri Mkuu MIZENGO PINDA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE ameruhusu ripoti ya tathimini ya rushwa nchini iwekwe wazi kwa wananchi ili umma uweze kufahamu ukubwa wa tatizo la rushwa nchini na chanzo chake kabla ya kujadiliwa na Baraza la Mawaziri.



Akizungumza wakati wa hafla ya ya kutiliana saini mkataba wa miaka mitano na wadau wa kimataifa wa maendeleo Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema kuwa ripoti hiyo itakapokamilika itatolewa ili iweze kutangazwa kwa umma na kasha kujadiliwa kwa kina.


Amesema ufadhili wa kukamilisha tathimini hiyo umefanywa na wadau hao wa maendeleo kutoka nchi mbalimbali duniani ambao walitaka kufahamu kiwango cha rushwa na maeneo ambayo inaonekana kuota mizizi.

No comments:

Post a Comment