Friday, May 13, 2011

MKUTANO UWEKEZAJI MAENEO HURU AFZA WAMALIZIKA LEO!

                                                           Bwana ADELHELM MERU (Kushoto)
Mkutano mkuu wa maeneo wa maeneo huru ya uwekezaji Afrika AFZA umemalizika leo jijini DSM huku maazimio ya mkutano huo yakiiishinikiza nchi za umoja wa Afrika AU kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuweza kufanikiwa katika uwekezaji pamoja na kupunguza changamoto zote zinazoikabili sekta ya uwekezaji.

Rais wa wa Maeneo huru ya uwekezaji Dokta NOBLE ADE amesema kuwa kama nchi za Afrika zikijiunga pamoja zinaweza kupiga hatua katika suala zima la uwekezaji na kuchangia bidhaa mbalimbali barani Afrika kuuzwa kwa wingi katika soko la dunia endapo pia suala la usindikaji likizingatiwa.


Kwa upande wa Mkurugenzi mkuu wa maeneo huru ya uwekezaji nchini EPZA Bwana ADELHELM MERU amesema pamoja na nchi nyingi za Afrika kujitangaza kutokana na rasilimali zake lakini hazijafanikiwa kupata maendeleo kwa sababu ya wawekezaji wachache hali inayochangiwa na kutokuwepo kwa mikakati madhubuti inayotumiwa na nchi zingine zilizoendelea.

No comments:

Post a Comment