Thursday, May 26, 2011

MKE WA MAKAMU WA RAIS AZINDUA MFUKO WA KUSAIDIA WAZEE WASIOJIWEZA!


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza wakati akisoma hotuba yake ya uzinduzi rasmi wa Mfuko wa kusaidia Wazee wasiojiweza wa ‘Pamoja Tushikamane’ ulio chini ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tushikamane Pamoja Faundation. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana Mei 24.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (katikati) na Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tushikamane Pamoja Faundation, Rose Mwapachu (kulia) wakipiga makofi kuwashangilia watu waliojitolea kuchangia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfuko huo iliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam jana Mei 24.
Baadhi ya Masister waliohudhuria hafla hiyo walioongazana na mmoja kati ya wazee wasiojiweza wanaomlea katika kituo chao Msimbazi.

                      Baadhi ya wahudhuriaji ya hafla hiyo wakifuatilia tukio hilo lililvyokuwa likiendelea
Mtunza hazina wa mfuko huo akionyesha kidani cha Silver alichonunua kwa Sh. 750,000 baada ya kupigwa mnada, ambacho thamani yake halisi ilikuwa ni Sh. 150,000. PICHA ZOTE NA MUHIDINI SUFIAN-OMR.

No comments:

Post a Comment