Friday, May 13, 2011

DOVUTWA AWASHUKIA DK SLAA NA MCH MTIKILA KISA RIDHIWAN KIKWETE!

                                                                 FAHMI DOVUTWA
Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP) kimesema kinaunga mkono Hatua iliyofikiwa na Mjumbe wa UVCCM taifa RIDHWAN KIKWETE ya Kutaka kuwafungulia mashtaka Katibu Mkuu (CHADEMA) Dakta WILBROAD SLAA pamoja na Mchungaji CHRISTOPHER MTIKILA kwa kumtuhumu kwamba yeye ni Fisadi.



Kauli hiyo imetolewa jijini DSM na Mwenyekiti taifa wa Chama Hicho FAHMI DOVUTWA wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Sakata hilo.


Amesema UPDP inaunga mkono hatua hiyo kutokana na Viongozi hao wa Kisiasa kushindwa kuangalia Changamoto na Matatizo mbalimbali ya wananchi kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa na badala wamejikita katika kutoa shutuma zisizokuwa na msingi wowote.

No comments:

Post a Comment