Moja ya foleni nchini NIGERIA
Waziri wa Fedha wa Nigeria NGOZI OKONJO-IWEALA na Waziri wa zamani wa Fedha wa Colombia JOSE ANTONIO OCAMPO wanatarajiwa kutajwa kama watu waliopendekezwa kugombea nafasi ya kuiongoza Benki Kuu ya Dunia.
Taarifa za kupendekezwa kwa OKONJO-IWEALA na OCAMPO, ambao wana ujuzi mkubwa wa masuala ya Uchumi na Diplomasia, zinaleta changamoto kwa Marekani kwani haijawahi kuwa na mtu wa kuwania nafasi ya kuiongoza Benki Kuu ya Dunia asiyetoka nchini humo.
Hata hivyo inatarajiwa kwamba mtu atakayechukua nafasi ya ROBERT ZOELLICK, ambaye kwa sasa ndiye Rais wa Benki Kuu ya Dunia, atatokea Marekani. Mtazamo huu unafuatia nchi ya Marekani kuungwa mkono na nchi nyingi, hasa zile za Ulaya. ZOELLICK ataacha madaraka yake mwezi Juni mwaka huu, kipindi ambacho muhula wake utamalizika.
Marekani imekuwa ikishikilia urais wa Benki Kuu ya Dunia tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo ya fedha baada ya vita kuu ya pili va dunia.
No comments:
Post a Comment