JULIUS MTATIRO
Chama cha Wananchi (CUF) kimeendelea kukumbwa na migogoro baada ya hii leo Wanachama wengine watatu kutangaza kujivua uanachama pamoja na kujiuzulu nyadhifa zao zote ndani ya chama hicho, akiwemo Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Vijana Taifa, Bwana OMARY COSTANTINE.
Wajumbe wawili wa Baraza kuu la Chama cha Wananchi (CUF), pamoja na Mkurugenzi wa Sekretariet ya vijana wa Chama hicho, wametangaza kujiondoa katika nafasi zao za uongozi ikiwemo kujivua uanachama kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa Chama hicho.
Katika madai yao wanachama hao walijivua magamba wamesema kutoridhishwa na mwenendo wa Chama hicho huku wakimtupia madai Katibu Mkuu wa CUF Bara, JULIUS MTATIRO kwamba anatumia jina lisilo lake.
Sambamba na hilo mmoja wa Wajumbe hao, Bwana ABUBAKAR RAKHESH amemtuhumu Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, kuwa jina analotumia la JULIUS MTATIRO sio jina lake halisi.
Akijibu tuhuma hizo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Bwana JULIUS MTATIRO, amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote. akitoa uthibitisho wake ikiwemo cheti cha kuzaliwa, vyeti vyake vya elimu ya juu na vile vya Chuo kikuu amesema majina yote anayoyatumia ni yake na hayana utata wowote.
Akienda mbali zaidi Mtatiro amesema wanachama hao waliojitoa walikuwa kwenye kundi la watu wanaotakiwa kufukuzwa ndani ya CUF na hivyo ameshukuru kwa wenyewe kutangaza kujiuzulu.
Wengine waliotangaza kukihama Chama hicho ni pamoja na Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Vijana taifa, Bwana OMARY COSTANTINE, na JUMA KILAGAI ambae alikuwa Mjumbe wa Baraza kuu la CUF.
Hali ni tete ndani ya chama hicho na kilichobaki ni kwa Wanaeastafrica.blogspot.com kuendelea kusubiri kitakachofuta......Karibu.
No comments:
Post a Comment