Sunday, February 19, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA UTAFITI BINGWA WA MASOKWE DUNIANI, JANE GOODALL!


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakizungumza na Mtafiti bingwa wa Masokwe Duniani, aliyekaa nchini kwa miaka 50 akifanya utafiti wa Masokwe katika Mapori ya Gombe na Mahale, Jane Goodall, wakati alipofika Ikulu ndogo Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi kwa ajili ya mazungumzo jana Februari 18, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kitabu cha mtafiti bingwa duniani wa Masokwe, Jane Goodall, aliyefika Ikulu ndogo ya Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi jana Februari 18, 2012 kwa ajili ya mazungumzo. Jane amekaa nchini kwa miaka 50 akifanya utafiti katika mapori ya Gombe na Mahale yaliyopo mkoa wa Kigoma na Katavi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal,
akielekezwa na mtafiti bingwa Duniani wa Masokwe, Jane Goodall, kuhusu ishara anazozitumia kuwasiliana na Masokwe na jinsi ya kuzungumza nao, wakati alipofika Ikulu ndogo ya Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi jana Februari 18, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment