Mdhamini wa timu ya Yanga ya Jangwani jijini Dar es salaam Mama Fatma Karume akizungumza katika hafla ya timu hiyo kuimiza miaka 77 tangu kuanzishwa kwake iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock na kuhudhuriwa na wanachama na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu, huku mgeni rasmi akiwa Dk. Fenella Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo anayeonekana kulia katika picha kushoto ni baadhi ya wazee wa Yanga. Mama Fatma Karume alisema Yanga ni mzee wa miaka 77 lakini katika michezo anaweza kukimbia kwa kasi ileile ya kimichezo, hivyo akamuomba mola ili klabu hiyo izidi kupata mafanikio katika michezo. |
No comments:
Post a Comment