Sunday, February 12, 2012

REST IN PIECE WHITNEY ELIZABETH HOUSTON


 Marehemu WITNEY ELIZABETH HOUSTON Wakati alipokuwa msichana.


Whitney amewa influence wa wasanii wengi sana wakubwa kwa wadogo.Miongoni mwao ni Celin Dion,Mariah Carey,Ton Braxton,Christina Aguilera,Nelly Furtado,Jessica Simpson,Kelly Clarkson,Britney Spears,Ciara,Jenipher Hudson,Lady Gaga,Brandy,Mary J,Leona Lewis,Beyonce,Alicia Keys na wengine wengi ambao wote wanafanya vizuri kimuziki.
 
 Ikumbukwe kuwa Whitney ndio msanii aliyevunja record ya guiness book of record kwa kuwa msanii wa kike aliyewahi kupata tuzo nyingi kuliko wote.Mpaka mwaka 2010 alikuwa na jumla ya tuzo mbalimbali za muziki 415.
 
 Kwenye maisha yake yote alijaaliwa kupata mtoto mmoja tu wa kike Bobby Christina.

 
 Whitney na Michael Jackson walikuwa marafiki na walishafanya kazi kadhaa pamoja.Michael alikuwa King of Pop na yeye queen of pop.Wote ni ma Icon wa muziki na ambao hatunao duniani.

 Mwaka 2009 alitokea katika kipindi cha Oprah na kusema hadharani kuwa alikuwa akitumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu ilaameacha.


Katika picha hii whitney akiwa na mama yake mzazi Cissy mwaka 1984 wakati ndio anaanza kuingia katika muziki akiwa ni binti tu wa miaka 21.Yeye na mama wake walikuwa wakiimba katika night club ndio akaja kuvumbuliwa na boss wa arista records.Alikuwa na sauti ya pekee ambayo mfano wake hauelezeki.



Atakumbukwa kwa mengi sana lakini cha zaidi ni baadhi ya nyimbo zake  tamu zisizochosha kusikiliza  kama the greatest love of all,i have nothing,i wanna know,i will always love you,my love is your love,when you believe,i learn from the best,try it on my own na nyingine kibao.


 Masaa 12 Kabla ya Kifo chake WHITNEY HOUSTON alionekana kwenye Gari hili akiwa mwenye furaha pamoja na boyfriend wake.
 

Kwa muda mrefu amekuwa akipambana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.Kifo chake inasemekana kimetokana na drug overdose japo haijathibitishwa bado.Aligunduliwa kuwa amefariki na bodygurd wake akiwa amezama bafuni kwenye bathtub .Whitney alikuwa katika hotel ya Beverly Hilton ambapo alikuwa anatakiwa kuperfom muda mchache baadae katika concert ya pre grammy bash.Alifariki jana jumamosi saa 3:30 pm saa za huko Marekani akiwa na miaka 48.Ukiacha muziki nilipenda sana filamu alizowahi kucheza waiting to exhale,the preacher's wife,the bodyguard pia kuna filamu yake mpya ya mwaka huu inaitwa sparkle bado sijaiona maana ndio imetoka



 Mungu alitoa na mungu Ametwaa,Pumzika kwa Amani  dada yangu WHITNEY  ELIZABETH HOUSTON

PROFILE
Birth Name:WHITNEY ELIZABETH HOUSTON
Nick Name: Nippy The Prom Queen of Soul
Born:AUGUST 9,1963
Place:NEWARK,NEW JERSEY U.S.A.
Died:SATURDAY,FEBRUARY 11,2012.
Aged:48 yrs.



 
 

No comments:

Post a Comment