Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea seti ya vyombo vya nyumbani na taa inayotumia nguvu za jua toka kwa Mkurugenzi wa Home Shopping Centre Bw Gharib Saidi Mohamed ambaye kampuni yake imejitolea kugawa seti kama hizo pamoja na taa kwa kila familia 655 zilizohamishiwa Mabwepande baada ya kuathirika na Mafuriko katika bonge la Msimbazi. Bw Gharib pia ameahidi kujenga shule ya msingi ya eneo hilo pamoja na kituo cha polisi.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakioneshwa maeneo ya makazi mapya ya walioathirika na mafuriko katika bonde la Msimbazi walipotembelea eneo hilo.
Rais Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Kanali Pastory Kamugisha wa JWTZ aliyefariki juzi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao mkoani Kagera. Hafla hii imefanyika katika kambi ya jeshi ya Lugalo Jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Kamishana wa Magereza Elias Mtige Nkuku, aliyefariki juzi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao mkoani Singida. Hafla hii imefanyika katika bwalo la jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU.
Na Mwandishi Maalumu
Kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) imeahidi kujenga kituo cha polisi, vyomba 14 vya madarasa ofisi za walimu na chumba cha kulia chakula kwa ajili ya waathirika wa mafuriko watakaohamia Mabwepande nje ya jiji la Dar es Salaam.Mbali na ahadi hiyo HSC imetoa mifuko 2,000 ya saruji, vyombo vya ndani na taa za sola kwa familia zote 653 zitakazopatiwa makazi kwenye eneo hilo.
Hayo yalisema leo na Mkurugenzi wa HSC Gharib Said Mohamed mfupi kabla Kamati ya maafa mkoani hapa kumkabidhi rais Jakaya Kikwete mahema 203 yaliyojengwa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS). Bw Gharib amesema kwamba shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi na jengo la kulia chakula vitakamilika katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa.
“Kwa kweli mpaka sasa kwenye saruji, vyombo vya ndani na taa za sola tumetumia zaidi ya sh milioni 70 kuhusu ahadi ya ujenzi wa kituo cha polisi na shule mpaka sasa gharama yake hatujaijua hadi vitakapokamilika,” alisema Bw. Gharib.
Aliwaomba pia wadau wengine wenye nia ya kuwasaidia wananchi hao kujitokeza kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye maeneo mengine huku akisisitiza kwamba jukumu la kusaudua utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa wananchi linawahusu wote. Awali rais Kikwete aliitaka kamati ya Maafa inayoshughulikia waathirika hao kufikiria namna ya kuwapatia viwanja waliokua wapangaji kwenye nyumba zote zilizobomelewa kwa mafuriko huku akiitaka kamati hiyo kuwa makini katika ugawaji wa viwanja hivyo.
“Msipokua makini zoezi hili haliishi… mtaendelea kufanya hivi kila siku watajitokeza pia wasiostahili watakuja kudai viwanja,” alisema rais Kikwete muda mfupi kabla ya kukabidhiwa na kukagua mahema hayo. Aidha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa kushirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) watafanya usafi wa maeneo na kujenga mahema kabla ya waathirika hao kuhamia Mabwepande.
No comments:
Post a Comment