Monday, January 9, 2012

AUAWA KIGOMA KWA KUKATAKATWA MAPANGA NA KUCHOMWA MOTO KUTOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA!

Mtu mmoja ameuwa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiofahamika kasha kuuchoma moto mwili wake katika kijiji cha Basanza wilayani Kigoma kutokana na imani potofu za kishirikina.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma ACP Frasser Kashai amemtaja aliyeuawa kuwa nib w. Husein Thobias mwenye umri wa miaka 48 na kwamba tukio hilo limetokea January 5 mwaka huu majira ya saa tano usiku

Amesema watu hao wakiwa na silaha mbali mbali yakiwemo mapanga,mashoka na mikuki walivamia nyumbani kwa Husein Thobias mkazi wa kijiji cha Basanza ambaye ni mganga wa kienyeji na kuanza kushambulia nyumba yake kwa kuirushia mawe na kufanya uharibifu mkubwa


Baada ya kuona hivyo Husein Thobias alitoka ndani ya nyumba na kuanza kukimbia ili kunusuru maisha yake lakini alikamatwa na watu hao ambao walimuua kwa kumkatakata kwa mapanga na mashoka kasha kuuchoma moto mwili wake


Aidha kamanda Kashai amesema katika tukio hilo mwili wa mtu mwingine aliyetambulika kwa jina la Thobias Windeye mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Basanza aliyeuawa kwa kukatwa ulipatikana mita kumi toka nyumba ya Husein Thobias


Amesema mtu huyo alikutwa amekufa huku akiwa amevaa gunia na kinyago cha kuficha sura yake na alikuwa na simu ya mkononi ambayo inashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.Katika tukio hilo watu wengine watatu walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya wilaya ya Kasulu kwa matibabu zaidi


Kamanda Kashai amewataja majeruhi hao kuwa ni Athumani Manamba, Herman Johnface na Gerlad Juma wote wakazi wa kijiji cha Basanza wilayani Kigoma.Amesema sababu za mauaji hayo ni imani za kishirikina ambapo watu walikuwa wakimtuhumu bw.Husein Thobias kuwa ni mchawi na kwamba uchunguzi wa kuwabaini waliohusika katika mauaji hayo unaendelea.


Kamanda Kashai amesema hakuna watu waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo lakini jeshi la polisi linamhoji mwenyekiti wa kijiji cha Basanza bw.Abdul Mteheye.

No comments:

Post a Comment