Monday, November 21, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WALIOPATA AJALI KAGERA!


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa Fabian Massawe kufuatia vifo vya watu 18 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea juzi, Jumamosi, Novemba 19, 2011, katika eneo la Lusahunga, Biharamulo, Kagera.

Aidha, Rais Kikwete ametuma salamu za pole kwa watu wote 17 walioumia katika ajali hiyo ambako basi la Taqwa liligongana na lori kwenye barabara la Biharamulo-Ngara.


Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Mkuu huyo wa Mkoa, “ Nimepokea kwa masikitiko na huzuni habari za vifo vya wenzetu 18 waliopoteza maisha yao katika ajali ya basi la Taqwa. Kupitia kwako nawatumia salamu zangu za pole za dhati ya moyo ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza watu katika ajali hiyo,”


Ameongeza Rais Kikwete: “Wajulisheni kuwa niko nao katika uchungu mkubwa walionao katika kipindi hiki cha maombolezo. Waambie kuwa msiba wao ni msiba wangu pia. Nawaombeeni subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi ya Mungu. Namwomba Mwenyezi Mungu aziweka roho za marehemu pahali pema peponi. Amen.”


Ameongeza Rais Kikwete: “Kwa wenzetu walioumia katika ajali hiyo, nawatumia pole zangu nyingi. Nawatakia heri waweze kupona haraka ili warejee katika shughuli zao za kujenga taifa na za kujiletea maendeleo.”...............

DAWA MPYA YA UZAZI WA MPANGO 'MYCROGYNON FE' YAINGIA SOKONI KWA 1,700/-!

Dr.Projestine S.Muganyizi, Senior lecturer and Reproductive Health Consultant Head Department of Obstetrics’/Gynaecology presents during the launch of a new contraceptive known as Microgynon FE manufactured in Germany by Bayer HealthCare and imported to Tanzania by Phillips Distributors Ltd the launch ceremony took place recently in Dar es Salaam.
Mr. Frans Labuschagne, Managing Director for Bayer East Africa speaks during the launch of a new contraceptive called Microgynon at the New Africa Hotel recently.
Mr. Robert A.Mkane Country Representative for Bayer HealthCare –Tanzania welcoming pharmacists and guests to the launch of new contraceptive Microgynon Fe manufactured in Germany by Bayer HealthCare and imported to Tanzania by Phillips Distributors Ltd the launch ceremony took place recently in Dar es Salaam.
Microgynon® Fe - is now available in Tanzanian pharmacies at a significantly lower price as a result of an innovative public-private partnership between Bayer HealthCare and the United States Agency for International Development (USAID).

The Microgynon brand is the world’s most widely used oral contraceptive. The price enables middle-income couples to access a quality, affordable family planning product. The initiative promotes the benefits of family planning in improving the health of women and their children.

This partnership was successfully launched in Ethiopia in December 2010, Uganda in September 2011, and now in Tanzania in a ceremony with Bayer HealthCare, USAID, and the Ministry of Health and Social Welfare on November 18, 2011.



“The partnership is designed to make more affordable family planning choices available to women through the private sector and address the growing gap between the demand for contraceptives and the ability of governments and donors to provide commodities”, said Dr. Jörg Reinhardt, Chairman of the Board of Management of Bayer HealthCare.

Family planning allows couples to plan their families as they desire, reduces the risks from unwanted and/or high-risk pregnancies, and improves the health of mothers and their children by allowing time between pregnancies.


After the introduction of Microgynon® Fe in Ethiopia, Uganda, and Tanzania, the Bayer-USAID partnership plans to expand their initiative to several additional Sub-Saharan countries by 2014. USAID’s Deputy Mission Director, Mr. Daniel Moore, emphasized the importance of public-private partnerships in helping governments meet their Millennium Development Goals.

“We are pleased that this important initiative between USAID and Bayer HealthCare is being launched in Tanzania. The private sector has an important role to play in contributing to sustainable development, and in this case, by ensuring that Tanzanian women have access to a sustainable supply of quality, affordable oral contraceptives.”


“Combined oral contraceptives are 99% effective when used consistently and correctly. It also provides women with a reversible method that is easy to discontinue and has a rapid return to fertility. Microgynon® Fe is being used by millions of women around the world and is well known and trusted by medical professionals”, said Dr. Projestine Muganyizi. Women interested in finding out more information about Microgynon® Fe should talk with their nearest private healthcare provider.

VODACOM FOUNDATION YAJENGA MADARASA MAWILI IRINGA!

Haya ndiyo madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kwa kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation” kwa ajili ya shule ya sekondari ya Lipuli ya mkoani Iringa.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga akiongea na wazazi na wanafunzi wa kata ya Kalenga Mkoani Iringa wakati wa hafla ya kuwakabidhi msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 kwa shule ya sekondari ya Lipuli ya mkoani humo ,yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kupitia mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”Kulia ni Afisa Elimu wa Sekondari za Wilaya ya Iringa William Mkangwa na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule.
Afisa Elimu wa Sekondari za Wilaya ya Iringa William Mkangwa akikata utepe kuashiria kupokea msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kwa kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”kwa ajili ya shule ya sekondari ya Lipuli, iliyopo kata ya Kalenga mkoani Iringa, wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya kusini Jackson Kiswaga,Diwani wa kata ya Kalenga Ameria Galinoma na diwani viti maalum Shakila Kiwanga.
Mkuu wa mfuko wa kusaidia Jamii wa Vodacom Tanzania Yessaya Mwakifulefule akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lipuli iliyopo kata ya Kalenga mkoani Iringa Agness John,mara baada ya kukabidhi msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kupitia mfuko huo.Akishuhudia watatu kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo Alex Mwakiyanga akiwa na walimu wa shule hiyo.
 Wazee wa kabila la Kihehe, kata ya Kalenga mkoani Iringa wakimpa heshima ya kichifu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga kwa kumkabidhi mkuki baada ya kumvisha vazi la mgolole ikiwa ni heshima kubwa kwa mkoa huo wakati walipofika kukabidhi madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 katika shule ya sekondari ya Lipuli mkoani humo.

KCB TANZANIA YAOMBA WANAFUNZI WAWEZESHWE UBUNIFU!

Wanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya Sekondari Kangaye iliyopo Nyamagana jijini Mwanza wakifanya mazoezi ya kimaabara kivitendo wakati Benki ya KCB Tanzania ilipokabidhi msaada wa vitabu vya sayansi wenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 hivi karibuni.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Bi Christine Manyenye akiteta jambo na Afisa Elimu Jiji la Mwanza Sekondari Anne Alopa (Katikati) na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kangaye Josephine Mlundwa baada ya kuwakabidhi msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 kutoka benki hiyo hafla iliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
Baadhi wa wanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya Sekondari Kangaye iliyopo Nyamagana jijini Mwanza wakiigiza mchezo wa ukosefu wa vitabu mashuleni wakati Benki ya KCB Tanzania ilipokabidhi msaada wa vitabu vya sayansi wenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 hivi karibuni.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Bi Christine Manyenye akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kangaye Josephine Mlundwa baadhi ya vitabu vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 vilivyotolewa na benki hiyo wakati wa hafla iliyofanyika Nyakato jijini Mwanza hivi karibuni. Anayeshudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule Joseph Nyanda.
Meneja wa KCB Tanzania tawi la Mwanza Elias Mwakatobe akimkabidhi Afisa Elimu Sekondari Jiji la Mwanza Anne Alopa baadhi ya vitabu vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 vilivyotolewa na benki hiyo kwa shule ya sekondari ya Kangaye wakati wa hafla iliyofanyika Nyamagana jijini Mwanza hivi karibuni.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Bi Christine Manyenye akiwakabidhi kaka mkuu wa shule ya sekondari Kangaye Marwa Mang’ana, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kangaye Josephine Mlundwa na dada mkuu Grace Gimahenga baadhi ya vitabu vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 vilivyotolewa na benki hiyo wakati wa hafla iliyofanyika Nyamagana jijini Mwanza hivi karibuni.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Bi Christine Manyenye akiwaelekeza jambo baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kangaye baada ya benki hiyo kuikabidhi shule hiyo vitabu vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 wakati wa hafla iliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.

KCB Tanzania yaomba wanafunzi wawezeshwe ubunifu

Na Mwandishi wetu, Mwanza
Benki ya KCB Tanzania imeiomba serikali kuongeza vifaa vya kufundishia katika shule mbalimbali nchini ili kuwawezesha walimu nchini kuibua vipaji tofauti vya ubunifu walivyonavyo wanafunzi. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Bi Christine Manyenye hivi karibuni wakati akikabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya Sayansi vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 kwa shule ya Sekondari Kangaye iliyopo Nyamagana jijini Mwanza.


Akifafanua Manyenye alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia wanafunzi wengi wameonesha utayari kubuni vitu mbalimbali lakini wanashindwa kuendelea mbele kwa kukosa miongozo ya kufika watakapo. Vilevile aliongeza kuwa msaada huo wa vitabu vilivyotolewa na KCB Tanzania utawezesha wanafunzi wa Sekondari ya Kangaye kujifunza masuala mbalimbali yatakayowasaidia kubuni bidhaa mbalimbali ambazo sasa zinaagizwa kutoka nje ya nchi.


“Hivi sasa hata kalamu za kuandikia zinaingizwa kutoka nje, hili linasababishwa na wanafunzi kutowezeshwa kuwa wabunifu tangu wakiwa watoto. KCB Tanzania imeliona hili na kuamua kuwekeza katika kusaidia vitabu hivi vya kisayansi ili kukuza uelewa miongoni mwao,” Alisema Manyenye. Kwa upande wake Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Jiji la Mwanza Anne Alopa alisema shule nyingi nchini zinakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kiada licha ambapo serikali imekuwa ikijitahidi kulipatia ufumbuzi suala hilo.


Kutokana na hilo Alopa alitumia fursa hiyo kuipongeza Bodi ya Shule ya Sekondari Kangaye kwa kumtafuta mdhamini huyo ambaye tayari ameonesha nia ya kuendelea kuisaidia shule hiyo baada ya awali kujitokeza kupanda miti zaidi ya 3,000 shule hapo. “Naipongeza KCB Tanzania kwa kuanza kutekeleza ahadi zake za kuisaidia Kangaye, natoa wito kwa uongozi wa shule kuendelea kushirikiana na benki hii ili kuweza kupata misaada zaidi,” alisema Afisa Elimu huyo.


Naye Mkuu wa Shule hiyo Josephine Mlundwa alisema msaada huo wa vitabu kutoka benki hiyo umepunguza mahitaji kwa asilimia 30 na kwamba utawezesha walimu kuongeza kiwango cha ufundishaji kwa wanafunzi. Mbali na hayo alizitaja changamoto nyingine zinazoikabili shule hiyo kuwa ni umeme, maji, vifaa vya maabara, viti na meza za maabara na za walimu, majengo ya utawala, maktaba, vyoo, nyumba za walimu, maabara kwani sasa wanatumia vyumba vya madarasa kama maabara kwa kufundishia masomo ya Sayansi.

BENKI YA NIC YAJITOSA KUDHAMINI GOFU KUSAIDIA WENYE MATATIZO YA MACHO!

Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NIC Tanzania, James Muchiri (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Mikopo wa benki hiyo Bi Regina Mwengi, Prisalla Karobia na David Muthungu kabla ya kuanza kwa michuano ya gofu iliyoandaliwa na Lions Club na kufanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.
Priscilla Karobia ambaye ni mmoja ya wanacahama wa Kalbu yak Gymkhana akiangalia mpira baaada ya kuupiga wakati wa Mashindano ya Gofu yaliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana ili kusaidia watu wenye matatizo ya kuona ambapo benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.
Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NIC Tanzania, James Muchiri akiangalia mpira baaada ya kuupiga wakati wa Mashindano ya Gofu yaliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana ili kusaidia watu wenye matatizo ya kuona ambapo benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.
David Muthungu mmoja ya wachezaji wa gofu akiangalia mpira baaada ya kuupiga wakati wa Mashindano ya Gofu yaliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana ili kusaidia watu wenye matatizo ya kuona ambapo benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NIC Tanzania akiwemo Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NIC Tanzania, James Muchiri (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama Lions Club wakati wa michuano ya Gofu iliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ili kusaidia watu wenye matatizo ya macho. Benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.

BENKI YA NIC YAJITOSA KUDHAMINI GOFU KUSAIDIA WENYE MATATIZO YA MACHO!
Na Mwandishi Wetu

Benki ya NIC Tanzania kwa kushirikiana na Klabu ya Lions ya Jijini Dar es Salaam wamejitokeza kudhamini mashindano yak mchezo ya Gofu ili kusaidia watu wenye matatizo ya macho. Katika mashindano hayo benki hiyo imetoa jumla ya Dola za Kimarekani 2000 sawa na Shilingi Milioni 3.5 za Tanzania lengo likiwa ni kuinua afya za wananchi hususani wanaosumbuliwa na matatizo ya macho.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji zaidi ya 105, Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa NIC Bank Tanzania James Muchiri amesema ni matarajio yao kwamba udhamini huo utasaidia upatikanaji wa afya bora katika eneo wanalotoa huduma zake.


“Tunatarajia msaada huu ambao ni wa kwanza katika sekta hii ya michezo kupitia Lions Club utasaidia watu wenye matatizo wa macho katika maeneo watakayoenda kutoa huduma hiyo kama ilivyo kawaida ya wana Mzizima,” alisema Muchiri.


Mbali na hayo Mkurugenzi na Mtendaji huyo Mkuu wa NIC Bank Tanzania alisema inakadiwa kuwa zaidi yak watu milioni tatu nchini wanakabiliwa na upofu kutyokana na uwezo mdogo wa kifedha, miongoni mwao wakiwemo wanafunzi. Kutokana na hilo alisema watahakikisha wanajenga uhusiano mzuri baina yao na Lions Club katika kuunga mkono mchezo wa gofu na kuwahudumia wenye matatizo ya macho.


Nchini Benki hiyo ina matawi Harbour View Tower jijini Dar es Salaam, Mwanza and Arusha huku ikitoa huduma mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba nafuu.