Jamii imeshauriwa kujenga utamaduni wa kuwaunga mkono mashujaa wanaotumia muda wao kusaidia wengine katika kuboresha maisha yao na kuachana na dhana ya kutegemea wawekezaji kutoka nje ambao hawajui mazingira halisi ya jamii husika.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Mradi wa Jitolee Tanzania, EDMOND LYATUU wakati wa Utambulisho wa Uzinduzi wa Tuzo mpya za kwanza Nchini zijulikanazo kama ‘TANZANIA GIVES BACK’ zenye lengo la kuonyesha mchango mkubwa wa Watanzania wanaojitolea muda na ujuzi wao kusaidia jamii.
Kwa upande wake Muendeshaji wa kipindi cha njia panda kinachorushwa kupitia CLOUDS FM, ambao walikuwa miongoni mwa wadhamini wa mradi huo, DK .ISAAC MARO amesema jamii inatakiwa kubadilika na kutatua matatizo yao pindi yanapojitokeza.
No comments:
Post a Comment