Monday, December 12, 2011
RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPOTEMBELEA MAONESHO YA MIAKA 50 YA UHURU VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE 77 JIJINI!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mratibu wa Maafa katika Idara ya Uratibu wa Maafa , Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Gilbert Mkindi , alipotembelea banda hilo katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Desemba, 2011, Kushoto ni Mkurugenzi msaidizi (Oparesheni) Bibi. Nyancheghe Nanai, na kulia ni Mratibu Maafa Bw. Fanuel Karugendo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Afisa Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Brandon Maro alipotembelea banda hilo katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Desemba, 2011, Kushoto ni Mkurugenzi (Utafiti, Sera na Mipango) Bw. Joel Kyaruzi.
Rais kikwete akitembelea bustani ya wanyama pori katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii
Rais Kikwete akiangalia gramophone ya 'His Masters Voice' katika banda la Wilaya ya Moshi
Rais Kikwete akiangalia bonge la boga
Rais Kikwete akipata maelezo ya mashine ya kisasa ya kufyatulia matofali kwenye banda la JWTZ.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment