Sunday, November 13, 2011

UHURU CHATA YADHAMINI RUGBY HOPAK SCHOOL!

Vijana wachezaji wa mchezo wa Rugby katika shule ya Hopac iliyopo Kunduchi chini ya kocha Shaun Graham iliyodhaminiwa kwa kutengenezewa jezi zenye chata ya Uhuru. Chata ya Uhuru ni ubunifu wa wabunifu wa mavazi Ally Remtullah na Vida Mahimbo wanaofanyakazi kwa ushirikiano na kampni ya Adidas ya Italia kwa lengo la kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana hususan katika mchezo wa Rugby.
Mbunifu wa Mavazi Vida Mahimbo (aliyebebwa) sambamba na vijana wa Kunduchi Nights na Ally Remtullah (mwenye miwani) mara baada ya kukabidhi jezi kwa timu ya Rugby ya Hopac School.
Yes this is it' Wabunifu bingwa wa mavazi Tanzania Vida Mahimbo (kushoto) na Ally Remtulla (kulia) wakimkabidhi Shaun Graham jezi za timu ya mchezo huo mbele ya kamera ya MO BLOG. Shaun pia ni Mratibu wa klab ya watoto wa Salasala.
Fallback wa timu hiyo Niko Kaihua akishoo love ambapo amewawakilisha wachezaji wenzake na kutoa shukrani za dhati kwa Vida Mahimbo na Ally Remtulllah kwa kubuni chata ya 'UHURU' ambayo inatengeneza mavazi ya vijana na pia imewachapishia jezi za Rugby zinazotengenezwa kwa ushirikiano na kampuni maarufu ya ADIDAS ya Italia.

No comments:

Post a Comment