Wakazi wa kata ya Iselamaganzi Shinyanga vijijini, wamedai kuwa hawajawahi kusomewa ripoti ya mapato na matumizi ya maji yanayotoka ziwa Victoria tangu mradi huo uzinduliwe na Rais JAKAYA KIKWETE.
Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti, mmoja wa wakazi wa eneo hilo Bw. GABLIEL MADAHA, amesema tangu kuzinduliwa kwa mradi huo hakuna jitihada zozote zilizochukuliwa ili kuufanya uweze kuwafikia wananchi wengi zaidi na kupunguza msongamano mkubwa wa watu pindi wanapohitaji maji bombani.
Aidha kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Iselamaganzi, Bwana PAULO KULWA, alipotakiwa kujibu malalamiko hayo hakuonyesha ushirikiano.
No comments:
Post a Comment