Afisa Michezo na Utamaduni Ubalozi wa Brazil nchini Tanzania Lazaro Ngimba (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na warsha ya mchezo wa Kapoeira itakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mda wa siku mbili ambapo amesema leo warsha hiyo itaanza Saa 12 jioni na kesho ni Saa 8 mchana na baadaye Wanakapoeira watakutana Kituo cha Utamaduni cha Russia ambapo Watanzania Wake kwa Waume wamealikwa kushuhudia mchezo huo.
Na Theeastafrica BlogerKwa mara ya Kwanza mchezo wa Kapoeira ulizinduliwa nchini Tanzania Mwezi June mwaka jana na kwa jijini Dar es Salaam mafunzo ya mchezo huo yanafanyika katika kituo cha Fitness Centre Msasani jijini Dar es Salaam.
Kapoeira ni Utambulisho halali wa Utaifa wa Brazil na Alama madhubuti ya Wabrazil, hazina Muhimu ya Utamaduni wa Utu na Umoja na ni Sanaa ya Kibrazil ya Ulinzi na Kujikomboa kutumia akili na viungo vya kibinadamu.
Pia ni sehemu ya taaluma, fani na ujenzi maalum nchini Brazil na nchi zingine ambako imekubalika na kutambulika, hivyo inafundishwa na inachezwa katika nyanja mbalimbali na kuzingatiwa katika tafiti za viwango tofauti vikijumuisha na vya Shahada ya Uzamili (Master's Digrii) na Digrii ya Udaktari wa Falsafa kwenye masomo ya Anthropologia, Historia, Soshologia, Elimu na Elimu ya Viungo.
No comments:
Post a Comment