Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Al-Jazeera, aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, ameuawa katika mapigano kati ya vikosi vinavyomtii na vile vya Baraza la Mpito mjni Sirte, akiwa mbioni kuukimbia mji huo.
Machache unayopaswa kujuwa kuhusu Gaddafi:
· Jina lake kamili ni Muammar Muhammad Abu Minyar al-Gaddafi, alizaliwa tarehe 7 Juni 1942, katika mji wa Sirte, kaskazini magharibi ya Libya
· Aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 1969 na kuondoshwa madarakani na waasi walioungwa mkono na Jumuiya ya Kujihami ya NATO mwaka 2011
· Utawala wake wa miaka 41 unatajwa kuwa wa nne kwa urefu kwa utawala usiokuwa wa kifalme. Alijiita Kaka Kiongozi, Mlinzi wa Mapinduzi na Mfalme wa Wafalme
· Kituo cha Televisheni cha Al-Jazeera kimeripoti kuwa Gaddafi ameuawa tarehe 20 Oktoba 2011 baada ya kukamatwa kutokana na mapigano kati ya walinzi wake na wapiganaji wa vikosi vya Baraza la Mpito linaloongoza sasa Libya.
No comments:
Post a Comment