Kampuni zinazofanya biashara ya mafuta nchini zimekubaliana kurejesha mfumo wa pamoja wa kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje kwa kuunda bodi ya wakurugenzi ya kampuni tanzu itakayoshughulikia zoezi hilo.
Hayo yamebainishwa, mapema hii leo Jijini Dar es salaam, katika mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA), kwa lengo la kuzikutanisha kampuni zinazofanya biashara ya mafuta nchini,
Akizungumzia bodi hiyo, Kamishina Msaidizi anaeshughulikia petroli na gesi, Wizara ya Nishati na Madini, PROSPER VICTUS, amesema itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa meli bandarini ikiwa ni pamoja na kupungua kwa gharama ya mafuta nchini.
No comments:
Post a Comment