Mtandao wa Jinsia Sumbawanga IJEN umeiomba serikali kukomesha mara moja vitendo vya jamii kusuluhisha kesi za ubakaji na unyanyasaji kijinsia katika ngazi ya kifamilia, ili kudhibiti kutokea kwa vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya wanandugu kwenye familia zao.
Akisimulia mkasa wa mtoto wa miaka mitatu aliyebakwa kwenye kijiji cha Mranda wilayani Sumbawanga mjini, kwenye tamasha la kumi la jinsia linaloratibiwa na Mtandao wa Jinsia TGNP, Bw ISMAIL MWASONGOLE kutoka mtandao wa IJEN, amesema serikali isipochukua hatua stahiki vitendo vya ubakaji kwa watoto vitaongezeka.
Katika hatua nyingine mwanaharakati MWASONGOLE amepinga kitendo cha wafanyabiashara kwenye kijiji cha Mranda kuwadhurumu wakulima baada ya kupima mazao yao kwa kutumia ndoo ziliyeyushwa ili zipanuke.
No comments:
Post a Comment