Thursday, September 15, 2011

VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUCHAPISHA HABARI ZENYE MASLAHI KWA WANANCHI!

                                                                    THOMAS MIHAYO

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuachana na dhana ambayo imezoeleka ya kuchapisha na kutoa ujumbe kwa malahi yao binafsi bali vimetakiwa kuwa na ubunifu wa kuhabarisha na kukosoa jamii katika Nyanja mbalimbali ili kuleta manufaa katika taifa zima.

Akizungumza jijini Dar es salaam mwenyekiti wa kamati ya maadili wa baraza la habari Tanzania Jaji mstafu THOMAS MIHAYO amevitaka vyombo vyote vya habari nchini kama kioo cha jamii kuangazia matatizo na changamoto zinazoikabili jamii na kuacha dhana kuendekeza maswala mengine ambayo hayana masilahi na jamii


Aidha ameyataja matizo ambayo yameshindikana kutatuliwa katika jamii ambao bila kutumia ghalama nyingi yangetatuliwa na vyombo vya habari ni kama ukuzi na ulezi wa watoto katika madili yanayofaa kesi za watoto mitaani nia nyine nyigi za aina hii.

No comments:

Post a Comment