Katika kutekeleza agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, SHAMSI VUAI NAHODHA, Jeshi la Polisi mkoani Singida limeanzisha utaratibu wa kukagua magurudumu ya mabasi na malori yanayosafiri masafa marefu, kwa kutumia barabara kuu ya ukanda wa kati, ili kuthibiti tatizo la ajali.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Singida, MOHAMMED LIKWATA, wakati akiongoza ukaguzi wa mabasi na malori yanayosafiri kwa kutumia barabara hiyo amesema kuwa, zoezi hilo litakuwa endelevu na kwa magari yatakayobainika kuwa na kasoro hayataruhusiwa kuendelea na safari.
Baadhi ya abiria waliosafiri kutumia njia hiyo, wamepongeza Jeshi la Polisi mkoani Singida, kwa madai kuwa njia hiyo itasaidia sana kuokoa maisha ya wasafiri wanaotumia barabara hiyo.
No comments:
Post a Comment