Wakati huohuo Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na taasisi zingine kama vile TRA , Bodi ya Sukari , Uhamiaji , Wizara ya Viwanda na Biashara , TBS , Tume ya Ushindani na Mwendesha mashitaka mkuu wa serikali, limeandaa operesheni maalum ili kubaini na kuhakikisha kwamba sukari inapatikana katika soko la ndani kwa kiwango cha kuridhisha.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurungenzi wa Makosa Jinai, DCI ROBERT MANUMBA amewaonya wafanyabiashara wote wanao wanajihusisha kuficha sukari , kusafirisha nje ya nchi kinyume cha sheria ama kuuza sukari kinyume na bei elekezi iliyopangwa na mamlaka husika kuacha vitendo hivyo maea moja.
Katika hatua nyingine DCI MANUMBA amewaomba wananchi kuunga mkono juhudi hizo za serikali ili kuhakikisha tabia ya kufichwa sukari inayofanywa na baadhi ya wafanyabiashara inakomeshwa na kuwezesha bidhaa hiyo kupatikana kwa urahisi.
No comments:
Post a Comment