Waziri Mkuu MIZENGO PINDA ameahirisha kujadiliwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa na Waziri WILLIAM NGELEJA Bungeni baada ya baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuikataa.
Akizungumza bungeni mjini Dodoma Waziri Mkuu PINDA ameomba serikali ipewe wiki tatu kuirekebisha bajeti hiyo na kuiridisha ili isomwe upya.
Spika wa Bunge ANNE MAKINDA ameafiki kukataliwa kwa Bajeti hiyo akiita ni nyeti na wabunge kusema itakapokuja kusomwa tena iwe na majibu yak uhalisia na mipango inayotekelezeka.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya bunge la nchi hatua hii kufikiwa, ingawa huko nyuma bajeti kama mbili ziliondolewa kabla ya kusomwa.
No comments:
Post a Comment