Wednesday, July 20, 2011

WAREMBO KUPIMA UKIMWI NA KUTEMBELEA OFISI ZA MANISPAA YA ILALA!

Warembo kumi na saba watakaoshiriki kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Ilala 2011, jumatano saa nne asubuhi wakiongozana na viongozi wa kamati ya miss Ilala wataenda kwenye kituo cha Amref kilichoko Upanga kupima afya zao ikiwa ni njia ya kuhamasisha wananchi katika Jiji la Dar es salaam waweze kupima kama wameathirika na magonjwa mbali mbali ili waweze kuchukua za kujilinda na maambukizi zaidi au kuanza kutumia tiba.

Warembo wa Ilala wanaenda kupima maambukizi ya VVU kama njia ya kuunga mkono juhudi za serikali kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi kwa vitendo. Wanaomba vijana wenzao kwa wazee kujua kuwa vita ya kushinda ukimwi katika taifa letu si vita lelemama. Ni lazima kila mtu awajibike kwa kujua hali ya kiafya, kujizuia kufanya ngono kwa vijana au kufanya ngono nzembe.


Watakapokuwa kwenye kituo hicho, watapewa elimu juu ya kujiepusha na vitendo vinavyo weza kusababisha maambukizi ya ukimwi pia watapewa ushauri nasaha kabla ya kuchukuliwa kwa damu zao na kupimwa.Suala la kutoa matokeo ya vipimo hadharani litakuwa ni suala la mshiriki binafsi maana matokeo ya vipimo yatatolewa kwa kila mshiriki pekee yake.


Aidha warembo wa Redds Miss Ilala 2011, watapata fursa ya kutembelea ofisi za Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala na kujifuza shughuli mbali mbali zinazofanywa na Manispaa katika kuinua maisha ya wakazi wa Wilaya ya ilala. Pia watapata fursa ya kukutana na Waheshimiwa Madiwani.


Warembo watakaoshiriki ktka kinyang’anyiro cha kumtafuta Mlimbwende wa Ilala watajigawa kwenye kata 26 zilizoko kwenye Wilaya ya Ilala ili waungane na Waheshimiwa madiwani kushiriki katika shughuli za kijamii na kimaendeleo kwenye kata husika. Kwa hiyo baada ya kukutana na waheshimiwa madiwani tutapata ma miss tofauti kulingana na kata zilizoko kwenye Manispaa ya Ilala. km Miss Upanga, Miss Vingunguti, Miss Ukonga, Miss Kariakoo, Miss Kivukoni, Miss Pugu, Miss Chanika, Nk


Shindano la Redds Miss Ilala 2011, litafanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja siku ya Ijumaa 29 Julai 2011 na limedhaminiwa na Redds Original akiwa mdhamini Mkuu, Vodacom, Paradise City Hotel, Paris Pub, Tanzania standard Newspapers, Channel ten, Michuzi Blogspot, TV Sibuka, Fabak Fashion, Maisha Club, B2C company, Papazi entertainment,


Imetolewa na


Jackson Kalikumtima
Mwenyekiti
Kamati ya Miss Ilala

No comments:

Post a Comment