BEATRICE SHELLUKINDO (Kulia)
Serikali imeombwa kuchunguza zilikopelekwa fedha zaidi ya shilingi Bilioni moja zilizochangishwa na Mtendaji Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ili kukamilisha maandalizi ya uwasilishaji wa hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/2012.
Mbunge wa Kilindi CCM BEATRICE SHELLUKINDO amesema Bungeni Mjini Dodoma kwamba wakati serikali ikijahidi kukabiliana na tatizo la umeme nchini mtendaji huyo alipisha mchango wa Milioni 50/- kwa kila idara na taasisi ya Wizara hiyo ili kukamilisha mchakato huo.
Katika hatua nyingine amemuomba Waziri Mkuu kulisimamia kidete suala hilo kwani tayari Katibu Mkuu kiongozi alishatoa waraka wa kuzuia fedha kutolewa kwa wabunge.
No comments:
Post a Comment