Monday, July 18, 2011

OLE SENDEKA AHOJI SERIKALI KUENDELEA KUNG'ANG'ANIA KUTUMIA MITAMBO YA UMEME YA KUKODI!

                                         CHRISTOPHER OLE SENDEKA (Kulia)
Mbunge wa Simanjiro CHRISTOPHER OLE SENDEKA amehoji uhalali wa serikali kuendelea kung’ang’ania kutumia mitambo ya umeme ya kukodi badala ya kukunua yake isiyokuwa na gharama za uendeshaji inayoipunguzia uwezo Tanesco kutoa huduma kwa Watanzania.

Akichangia hoja ya Wizara ya Nishati na Madini Muheshimiwa OLE SENDEKA amesema kuna haja ya serikali kufunga mikanda na kupitisha azimio la dharula la kununua mitambo yake ya umeme ili kulinusuru taifa na mgao wa umeme.


Kuhusiana na mtambo wa kuzalisha umeme kutumia mafuta mazito wa Megawati 60 unaojengwa jijini Mwanza Mbunge huyo wa Simanjiro amesema, huo ni ufisadi mwingine unaoandaliwa na serikali.

No comments:

Post a Comment