Serikali ya Jahmhuri ya kidemokrasia ya Congo imetangaza siku tatu za maombolezo kwa watu waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege mjini Kisangani siku ya ijumaa. Akitangaza siku hizo msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bw. Lambert Mende alisema kuwa ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 72, na nchi hiyo itawaombolza watu hao waliofariki kwa siku tatu mfulilizo kuanzia tarehe 9.
Ajali hiyo ilitokea wakati ndege ya abiria aina ya Boeing 727 ya shirika la ndege la Hewa Bora ilipojaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kisangani. Hivi sasa pande husika bado zina maoni tofauti kuhusu idadi ya watu waliofariki katika ajali ya ndege.
Mfanyakazi wa ofisi ya idara ya usimamizi wa safari ya ndege ya nchi hiyo tawi la Kisangani alisema, kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha tarehe 8 mchana, ndege hiyo ilishindwa kudhibitiwa ikagonga miti iliyoko kilomita 1 mbali na njia, na kuwasha moto.
No comments:
Post a Comment