Monday, July 25, 2011
MAONESHO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU NA WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAINGIA SIKU YA PILI!
Maonyesho ya kuelekea kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania yaliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini yanaingia katika siku ya pili huku Wizara hiyo hikikiri kuwepo kwa uhaba wa gesi jijini Dar es salaam na baadhi ya maeneo mengine nchini.
Akizungumza na kituo hiki katika maonyesho ya Wiki ya Nishati na Madini, Mjiolojia Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini HABASS NG’ULILAPI amesema Wizara inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa gesi kutokana na viwanda kuwa na mahitaji makubwa hususani jijini Dar es salaam.
Aidha Ng’ulilapi ameongeza kuwa serikali imejipanga kutoa gesi nyingi kwa kujenga bomba kuu kutoka Mtwara mpaka Dar es salaam hadi Mombasa ikiwa ni lengo kubwa la kupanua wigo wa gesi Nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment