Vijana nchini wametakiwa kubadilika na kupiga vita mauaji ya vikongwe nchini kutokana na imani za kishirikina baada ya vitendo hivyo kuendelea kutokea licha ya Serikali kuuelimisha umma kujiepusha na suala hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi SHAMSI VUAI NAHODHA akitoa ufafanuzi kuhusiana na kuendelea kwa vitendo vya mauaji ya vikongwe amesema ili kukomesha kabisa vitendo hivyo jamii iunge mkono kwa kuwaelimisha vijana kuachana na imani za kishirikiana.
Akijibu swali la msingi Bungeni mjini Dodoma Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi HAMIS KAGASHEKI amesema kuanzia mwaka 2005 hadi kufikia 2010 jumla ya vikongwe 2,500 waliuawa kwa kuhusishwa na imani za kishirikiana.
No comments:
Post a Comment