Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 45 na kufikishwa mahakamani baada kufanya misako mbalimbali na kukamata silaha za kivita,risasi,pamoja na silaha za kiraia,katika kipindi cha mwezi mmoja.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo JUSTUS KAMUGISHA amesema kuwa mbali na kukamata silaha hizo vilevile jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata pombe haramu ya moshi lita 740, pamoja na mitambo minne ya kutengenezea pombe hiyo, ambapo watuhumiwa 20 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani baada ya kukamatwa na pombe pamoja na mitambo ya kutengenezea pombe hiyo haramu ya moshi.
Aidha katika misako hiyo pia watu sita walikamatwa na kufikishwa mahakama baada ya baada ya kukutwa na jumla ya kilo 318 za bhangi,na kwamba jeshi la polisi lilifanikiwa kuteketeza ekali tatu za bhangi ambazo zilikuwa zikimilikiwa na watuhumiwa hao.
No comments:
Post a Comment