Wednesday, July 20, 2011

RAIS KIKWETE ASEMA MATAIFA YA AFRIKA YANAHITAJI MISAADA YA KIMAENDELEO!

Rais JAKAYA KIKWETE amesema mataifa ya Afrika bado yanahitaji misaada ya Ki-maendeleo, ingawa wajibu wa kujiendeleza unabakia mikononi mwao na sio kwa mataifa ya Kigeni wakiwamo wafadhili.

Rais KIKWETE ambae yupo Afrika Kusini kwa ziara ya Kihistoria tangu taifa hilo lilipopata uhuru mwaka 1994, amewataka wafanyabiashara na wawekezaji nchini humo kuanzisha vitega uchumi na kuwekeza katika uchumi wa Tanzania kwa sababu ya vivutio vikubwa vilivyopo hapa nchini.


Amesema umefika wakati kwa Tanzania na Afrika Kusini kutumia uhusiano wa kihistoria ili kujenga mahusiano imara na ya karibu zaidi ya kiuchumi baina ya nchi hizo.


Hadi sasa kiasi ya makampuni 178 ya Afrika Kusini yamewekeza katika uchumi wa Tanzania kwa thamani ya kiasi cha dola za Marekani milioni 592.82. Miradi hiyo imetengeneza kiasi cha ajira 18,438 kwa ajili ya Watanzania.

No comments:

Post a Comment