Serikali imeazimia kufanya mageuzi katika matumizi ya Sindano kufuatia kuwepo kwa matumizi mabaya ya kifaa hicho kwa mgonjwa zaidi ya mmoja.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, DK. LUCY NKYA akizungumza baada ya kupokea msaada wa kontena la sindano zenye uwezo wa kujiharibu baada ya kutumika, kutoka Asasi isiyo ya kibiashara ya SAVE POINT amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia sindano moja kwa kushirikiana.
Lengo la mageuzi hayo ni kuzuia matumizi ya kifaa hicho kwa mgonjwa zaidi ya mmoja na kwamba sindano hizo zitauzwa kwa gharama ndogo ili kila mwananchi amudu gharama yake.
No comments:
Post a Comment