Mkuu wa Wilaya ya Ilala, LEONIDAS GAMA, ametoa wiki mbili kwa Manispaa zote tatu Jijini Dar es salaam kutatua tatizo la taka katika dampo lililoko eneo la Pugu Kinyerezi jijini.
GAMA, amesema dampo hilo limekuwa moja ya kero kubwa za usafi na mazingira na kwamba wakazi wa eneo hilo wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na dampo hilo kujaa taka kupita kiasi.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amepokea vifaa mbalimbali vya usafi kutoka Kampuni ya TBL, ikiwa ni maandalizi ya Siku ya Mazingira duniani inayotarajiwa kuadhimishwa June 5 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment