Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kupunguza vifo vya watoto na akina mama wajawazito nchini, Kampuni ya Phillips Tanzania imeandaa semina ya siku tatu kwa manesi na madaktari bingwa wa watoto ili kuwapa mafunzo wauguzi hao kugundua matatizo yanayomkabili mama mjamzito na mtoto wake kabla hajajifungua.
Mwakilishi wa Phillips Health Care, MONICA JOSEPH amesema kupitia mafunzo hayo washiriki hao zaidi ya 140 watakuza uelewa wao katika kutoa huduma za mama na mtoto lengo likiwa ni kupunguza vifo vya watoto vinavyotokea wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mshauri Mwandamizi Hospitali ya Mkoa DK FREDRICK MLEKWA amesema mafunzo hayo ni muhimu hususani kwa watoa huduma wa afya walioko pembezoni ambao wamekuwa hawafikiwi na semina elekezi za mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment