Tuesday, June 14, 2011

WANAFUNZI MUHAS WAGOMA KUPINGA KUFUTWA KWA CHAMA CHA WANAFUNZI!

Wanachuo wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Muhimbili (MUHAS), Jijini Dar es salaam, hii leo wameandamana mpaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kufuatia madai yao ya Msingi kutotekelezwa na uongozi wa Chuo hicho ikiwa ni pamoja na Kufutwa kwa Chama cha Wanafunzi Chuoni hapo.

Akizungumza na kituo hiki, Jijini, Rais wa Chuo hicho, GERVAS SHAYO, amesema wamelazimika kuchukua uamuzi huo kufuatia kutolizishwa na kanuni zilizotumika katika mchakato wa kufuta Chama hicho na kwamba kanuni hizo ni kandamizi.
Hata hivyo Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova alifika katika eneo hilo na kufanikiwa kuwatuliza wanafunzi hao baada ya kuwasihi kukaa na kusubiri majibu ya Madai yao.
Wakati huo huo Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia Mkoani Dodoma mapema hii leo walilazimika kutumia mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya wanafunzi wa wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatanya Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM wa vitivo vya Sayansi za Jamii, sanaa ya lugha na Sayansi asilia waliokuwa wakifanya maandamano kuelekea Bungeni.
Kamanda wa upelelezi na makosa ya jinai mkoani humo SAFIEL MKONYI amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza tayari baadhi ya wanafunzi wameshakamatwa kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment