Benki ya KCB Tanzania kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha Chanika- Msolongola imeendesha zoezi la kupanda miti zaidi ya 9000 ili kuadhimisha siku ya jamii ambapo kila mwaka hugusa moja ya sekta ambazo benki hiyo husisaidia.
Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa, amesema zoezi hilo linalenga kuiunga mkono serikali katika suala la utunzaji wa mazingira na kwambawamepanga kupanda miti 21,000 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Morogoro na Arusha.
Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Msongola ANGELINA MALEMBEKA amesema kupitia baraza la kata hiyo atahakikisha miti hiyo inatunzwa na kuhudumiwa na yeyote atakaebainika kuiharibu atashitakiwa kwenye baraza hilo.
No comments:
Post a Comment