Prof. Ibrahim Lipumba akiingia kituo kikuu cha Polisi kumwekea dhamana iliyoshindikana Mbowe
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), PROF. IBRAHIMU LIPUMBA, amesema taasisi hiyo inatarajia kufanya mkutano kujadili hali ya Demokrasia nchini kufuatia baadhi ya Wabunge kuwekwa kizuizini akiwemo mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), FREEMAN MBOWE.
Akizungumza Jijini Dar es salaam, PROF LIPUMBA, amesema kuna haja ya bunge kuweka utaratibu mzuri utakaowalinda Wabunge na kwamba taasisi hiyo inatarajia kutoa tamko katika mkutano utakaofanywa na taasisi hiyo, kufuatia kukamatwa kwa wabunge hao.
Aidha ameongeza kuwa Chama cha Wananchi (CUF), kinatarajia kufanya maandamano June, 12 mwaka huu, kupinga mauaji yanayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba maandamano hayo yataanzia Makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujona (Ubungo Mataa) na Kuishia Viwanja vya Manzese.
No comments:
Post a Comment