Sunday, June 5, 2011

JIJI LA DAR ES SALAAM LAONGOZA KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NCHINI!

Tanzania hapo jana iliungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ongezeko la watu pamoja na uelewa mdogo juu ya utunzani wa mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, LEONIDAS GAMA, amesema uharibifu wa mazingira katika Jiji la Dar es salaam kwa sasa unatisha ukilinganisha na Miji mingine nchini kufuatia wananchi wengi kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya utunzaji wa mazingira.
GAMA ameongeza kuwa maisha ya wananchi kwa ujumla yana uhusiano mkubwa na mazingira kufuatia uhai wa binadamu kutegemea zaidi mazingira safi na salama huku maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Panda Miti na Kuitunza Hifadhi Mazinghira,’ kitaifa yakifanyika Mjini Songea, Mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment