Saturday, June 4, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA MATAIFA YA TROPIKI YALIYO UKANDA WENYE MISITU MIKUBWA!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo jijini Brazzaville, jana Ijumaa, Juni 3, 2011 kuhudhuria Mkutano wa 3 wa Nchi za Tropiki zilizo katika ukanda wenye misitu mikubwa na mvua nyingi. Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka katika nchi zaidi ya 30 zilizo katika ukanda huo, mataifa yaliyoalikwa sambamba na mashirika ya Kimataifa yanayoshughulika na masuala ya mazingira.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya marais wa nchi mbalimbali katika mkutano wa Mataifa ya Tropiki yaliyo katika Ukanda wenye Misitu mikubwa na yenye kuvuna mvua kwa wingi, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo Brazzaville jana Ijumaa Juni 3.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake katika Mkutano wa Mataifa ya Tropiki yaliyo katika Ukanda wenye Misitu mikubwa na yenye kuvuna mvua kwa wingi, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo Brazzaville jana Ijumaa Juni 3.
Kutoka (kushoto) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Waziri katika ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Fatma Fereji na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, wakiwa katika mkutano huo, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo Brazzaville, jana Ijumaa Juni 3.
Picha ya pamoja ya Marais wan chi balimbali waliohudhuria mkutano huo leo Juni 3 Jijini Congo Brazzaville. Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment