Sunday, June 5, 2011

KIKOSI CHA ZIMAMOTO JIJINI DSM CHAMALIZA UTATA WA KUZAMA KWA MTOTO CHOONI!

Kikosi cha zimamoto kwa kushirikiana na wananchi wa eneo ya Ubungo Makuburi jijini Dar es Salaam mapema hii leo walikuwa katika wakati mgumu wakutafuta mwili wa mtoto aliyedaiwa kutumbukia katika shimo la choo cha shule la Msingi Makuburi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema watoto watatu waliingia katika choo hicho na muda mfupi baadae walipiga kelele kwamba mwenzao mmoja ametumbukia katika shimo la choo.
Kamanda wa zamu wa Kikosi cha Zimamoto cha Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Sajenti Meja SAIDI KILIMALI amesema jitihada za kikosi chake za kutafuta mwili huo zimegonga mwamba na hawakumpata mtu ndani ya choo hicho.

No comments:

Post a Comment