Tuesday, June 7, 2011

CUF YALAANI MAHAKAMA WILAYANI URAMBO TABORA KUWANYIMA VIONGOZI WAKE DHAMANA!

Chama cha Wananchi CUF kimelaani Vikali hatua iliyochukuliwa na mahakama wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora ya kuwanyima Dhamana Viongozi waandamizi wa Chama Hicho kwa kuwapa masharti magumu yasiyotekelezeka.

Sanjari na hatua hiyo Chama hicho kimepanga kufanya maandamano makubwa ya Amani June 12 kwa lengo la kupinga hatua ya jeshi la polisi pamoja na Viongozi wa Serikali Wilayani humo kuendelea kuwanyanyasa wananchi kwa kuwatishia na kuwapora mifugo yao kinyume na Utaratibu.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini DSM Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa IBRAHIM LIPUMBA pia Amezitaka Taasisi zinazojishuglisha ufuatiliaji wa Haki za Binadamu kuingilia kati suala hilo.

No comments:

Post a Comment