SACP MOHAMED MPINGA
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali “Investment Climate Facility for Africa-ICF” limebuni mradi utakaohakikisha kunakuwepo na usalama wa mizigo inavyosafirishwa kwenye barabara kuu za nchini.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani SACP MOHAMED MPINGA amesema mradi huo kwa kiasi kikubwa utafanikisha usalama wa mizigo inayotoka nje na ndani ya ikiwa ni pamoja na kupunguza vitendo vya rushwa vinavyofanywa na askari wa usalama barabarani.
Kwa awamu ya kwanza mradi huo utaanzia kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam hadi Rusumo mkoani Kagera mpakani mwa Rwanda na Tanzania.
No comments:
Post a Comment