Thursday, June 23, 2011

HABARI ZA BUNGE KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA!

                         SERIKALI YAKATAA KUDHALISHWA NA BAE SYSTEMS!
Serikali imesema haitokubali kushuhudia ikidhulumiwa kiasi cha pauni za Uingereza milioni 29.5 sawa na shilingi bilioni 74 inazozidai kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Uingereza (BAE Systems) na kwamba iko tayari kulinda heshima ya Tanzania katika medani za kimataifa.

Akiwasilisha kauli za Mawaziri leo hii Bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, BENARD MEMBE amesema ingawa Tanzania ni taifa masikini lakini haiku tayari kudharauliwa na kwamba kuruhusu fedha hizo kupewa asasi ya kiraia ni sawa na kukubali kuibiwa kwa mara ya pili.
Hivi karibuni Kampuni hiyo ya Ulinzi ya Uingereza (BAE Systems) ilisema italipa jumla ya bilioni 74 inazodaiwa na serikali kwa kuipa asasi isiyo ya kiserikali ya nchi hiyo ili kufanya shughuli za hisani nchini badala ya kuilipa Tanzania moja kwa moja kama ilivyoamriwa na Mahakama nchini humo.

   KAMBI YA UPINZANI BUNGENI YALISHAWISHI BUNGE KUONGEZA MUDA WA CHC!
Kambi ya Upinzani Bungeni imefanikiwa kulishawishi Bunge kupitisha azimio la serikali la kuongeza muda wa utendaji kwa Shirika Hodhi la Consolidated Holding Corporation (CHC) lililopewa jukumu la kukusanya madeni yaliyotokana na ubinafsishaji wa mashirika ya umma.

Akichangia mada kuhusiana na hoja hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini ZITTO KABWE amesema kutokana na shirika hilo kufuatilia madeni ya takribani mashirika ishirini na tano ya kuwepo kwa ukiritimba katika ubinafishaji kuna budi kwa serikali kutolivunja shirika hilo.
Baada ya hoja hiyo iliyotolewa na ZITTO KABWE na wabunge wengine wa ikiwemo wa Chama cha Mapinduzi CCM, Waziri wa Fedha MUSTAPHA MKULO anasema….

Akiwasilisha azimio la serikali Bungeni, Waziri MKULO aliiomba serikali kuongeza muda wa mpito wa miaka mitatu kwa shirika Shirika Hodhi la Consolidated Holding Corporation (CHC) hilo ili serikali iweze kuhamisha kazi zilizobaki kutoka CHC na kuzikabidhi kwa ofisi ya Hazina.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini ZITTO KABWE ametoa rai kwa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wote kwa ujumla kuwa na moyo wa uzalendo katika kusimamia mali za serikali ili kuwakomboa wananchi kuondokana na umasikini.

Akichangia hoja ya azimio la serikali Bungeni mjini Dodoma kuhusiana na hoja ya kuongeza muda wa mpito wa utendaji kwa Shirika Hodhi la Consolidated Holding Corporation (CHC), KABWE ameomba bunge kuwa na jicho la kuhakikisha mali zote za umma hazipokwi na mafisadi.


Shirika Hodhi la Consolidated Holding Corporation (CHC) ndilo lililopewa jukumu la kukusanya madeni yaliyotokana na ubinafsishaji wa mashirika ya umma ikiwemo iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

No comments:

Post a Comment