Wakati Rais JAKAYA KIKWETE akihimiza viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kuacha kufanyia kazi zao ofisini, hali hiyo ni tofauti katika eneo la Sinza C baada ya wakazi wa eneo hilo kuilalamikia ofisi ya serikali ya mtaa huo kushindwa kuzoa taka zilizorundikana kwenye jalala la mtaa huo.
Lakini suala hilo linaonekana kama ni la tofauti, kwani Manispaa ilishaweka tangazo kwa eneo hilo kutomwaga taka na atakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo faini ya shilingi 300,000/-Baadhi ya wakazi kwa kukosa eneo la kumwaga taka, wanatumia fursa ya tela la Manispaa hiyo lililopo jalalani hapo kumwaga takataka zao.
Hili ndilo tangazo lililowekwa na Manispaa ya Kinondoni linavyoonekana leo hii, tafakari dhana ya tangazo hilo na kitendo cha taka kuendelea kumwaga katika eneo hilo!
Baadhi ya takataka hizo za wakazi wa Sinza C zikisubiri gari za kuja kuzichukua, kama amri imeshatolewa trela hili ni la nini katika eneo jalala hili lililopo pembezoni mwa ukuta wa Chuo cha Posta?
Mwanaeastafrica hakuona shime kwenda kupata ufafanuzi juu ya amri hizo mbili zinazosigana kati ya serikali ya mtaa huo na ile ya Manispaa ya Kinondoni, wanaoendelea kuathirika ni wakazi wa Sinza C, je hao wanahusika na magonjwa ya mlipuko kutokana na mlundikano wa takataka hizo!
Huyu ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Sinza C Bwana OMARI MAGEMBE akilitolea ufafanuzi suala hilo......
Wakizungumza na kituo hiki, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema serikali ya mtaa huo umekiuka utaratibu uliojiwekea wa kukusanya taka kwenye nyumba zao jambo linalohatarisha usalama wa afya zao hususani katika kipindi hiki cha mvua za masika kwa kupata magonjwa ya milipuko.
Akizungumzia hali hiyo Mwenyekiti wa Mtaa wa Sinza C, OMARI MAGHEMBE amesema kasi ya uzoaji taka inayolalamikiwa inachangiwa na mvua na kwamba magari yanashindwa kufika katika kituo cha kukusanyia taka kilichopo pembezoni mwa ukuta wa chuo cha posta.
No comments:
Post a Comment